
Leo katika dimba la Santiago Bernabeu wenyeji Real Madrid watakua na kibarua cha kuwakabili wababe Barcelona katika mechi ya raundi ya pili ya kumtafuta mshindi wa Super Cup.
Ikumbukwe wiki moja iliyoipita timu hizi zilikutana katika dimba la Camp Nuo, katika mchezo ulioishuhudia Real Madrid ikiendelea kuwa mteja wa Barca kwa kula kipigo cha 3-2.
Real ina kabarua kigumu leo kwanza wa kitaka kuwaondoa hofu mashabiki wa trimu hiyo kutokana na mwanzo mbaya katika La Liga msimu huu, na pia kuondokana na uteja wao kwa Barca.
Nani atakayeibuka na ushindi? ni swali ambalo kila shabiki wa soka anajiuliza lakini dakika 90 au 120 ndizo zitakazo amua mchezo huo maarufu kama El Classico.!
No comments:
Post a Comment