Search This Blog

Sunday, August 19, 2012

ALEXANDER SONG NJIANI KUELEKEA BARCELONA!

Alex Song

Mchezaji wa kimataifa wa Cameroun,  na anayachezea Arsenal ya Ligi kuu ya Uingereza {EPL},Alexander Song {juu pichani} atakua mchezaji mwingine mwenye jina kubwa kuihama kilabu hiyo ya kaskzini mwa London, na hiyo ni baada ya kilabu ya Arsenal na miamba wa Catalan, Barcelona kufikia makubaliano juu ya ada ya uamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ambayo ni pauni 15 milioni. Song atafuata nyayo za nahodha wa zamani wa kilabu  hiyo Robin Van Persie aliyetimukia kwa wapinzani Manchester United.

Akihojiwa na Goal.com Wenger alisema katika kutafuta mbadala wa Song kilabu hipo kwenye mchakato wa kupata deal na kiungo wa Real Madrid mturuki Nuri Sahin. "Ni mchezaji ambaye bado tunamfuatilia" alisema Wenger.

No comments:

Post a Comment