Nyimbo ya kushirikiana ya Msanii anayelipwa pesa nyingi kwa kupiga show nchini Diamond Platinumz na Msanii maarufu nchini Nigeria, J. Martins hiko njiani kukamilika baada sehemu kubwa ya nyimbo kuwa imefanyika.
Diamond amefunguka kuwa nyimbo hiyo imefanyika kwenye studio za MJ Records chini ya Prodyuza mkali nchini Marco Chali na pia katika nyimbo hiyo itasikika sauti ya ya Mose ambaye ni dancer wa Diamond.
Pia habari kutoka kipindi cha Power Jamz cha East Africa Radio ni kuwa Diamond na dancers wake wako njiani kuelekea Washington DC nchini Marekani ambako watapiga show katika jiji hilo.
No comments:
Post a Comment