Search This Blog

Sunday, August 19, 2012

MATOKEO YA JANA EPL: ARSENAL YASUA SUA!,.....

'Giroud can deal with Van Persie burden'


  1. Hiyo jana katika dimba la Emirates, vijana wa Arsene Wenger "The Gunners" wakiwa na wachezaji wapya waliosajili katika msimu wa majira ya joto walitoka sale ya bila kufungana na Sunderland a.k.a "Black Cats" wakiongoza na kocha mzoefu Martin O'neil. Arsenal wakiwa wenyeji wa mchezo huo walipata nafasi kadhaa lakini tatizo lilikuwa kutikisa nyavu za wapinzani wao, na hasa nafasi aliyoipata mchezaji mpya aliyesajiliwa kutoka Montpellier, Giroud katika dakika za mwisho za mchezo huo na kupoteza nafasi hiyo ya wazi.
EPL; Peter Odemwingie, West Bromwich Albion v Liverpool

2. Huko Hawthrons, dimba la nyumbani la West Bromwich ilikuwa ni vita ya katika ya kocha mpya wa wenyeji Steve Clarke na kocha mpya wa The Reds, Brendan Rodgers. Pamoja na usajili uliofanywa na Rodgers haukuondosha kipigo cha 3 kwa kutoka kwa wenyeji West Brom. Liverpool ikicheza na wachezaji kumi dimbani baada ya beki Daniel Agger kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumchezea visivyo Shayne Long na refa kuamuru upigwe mkwaju wa penati ambapo Long alikosa penati hiyo. Magoli ya wenyeji yalifungwa na Gera, Peter Odemwingie na Romelu Lukaku aliyeko kilabuni hapo kwa mkopo akitokea The Blues alifunga goli la mwisho na kuhitimisha mwanzo mbaya kwa Brendan Rodgers.


EPL; Michu, Queens Park Rangers v Swansea City

3.Katika dimba la Loftus Road Stadium Michael Laudrup akiwa kocha mpya EPL na kwa timu yake ya Swansea City alianza kazi yake kwa furaha baada ya kuiangaushia QPR chini ya Mark Hughes kipigo cha mbwa mwizi cha magoli 5 bila majibu ugenini.Kiungo mshmbuliaji mpya Michu raia wa hispania alianza kuitimika kilabu yake vyema baada ya  kufunga mawili na Dyer akifunga magoli mawili pia huku sherehe ya mabao ikihitimishwa na Sinclair aliyeingia kuchukua nafsi ya Dyer.  

EPL - Newcastle United v Tottenham Hotspur, Aaron Lennon, Davide Santon and Jonas Gutierrez

4. Huko St James Park, wenyeji Newcastle Utd waliwakaribisha Totenham Hotspurs walio chini ya uongozi
wa manager mpya A.V Boas na katika mchezo huo wenyeji Newcastle chini ya Allan Pardew walichomoza na ushindi wa 2-1 dhidi ya wageni kutoka White Hartlane. Wenyeji ndo walianza kupata goli kupitia kwa Ba katika dakika ya 45 kipindi cha pili kwa shuti kali lililokwenda katika kona za juu za goli lililokuwa likilindwa na Tom Briedefil, lakini katika ya 76 J. Defoe aliisawazishia Hotspurs ila shukrani zilienda kwa Ben Arfa alifunga kwa penati baada kuangushwa kwenye box na Lennon na kuandika ushindi wa kwanza kwa Newcastle msimu huu. 

No comments:

Post a Comment