
Jana usiku kwenye Monday Night Football katika dimba la Goodson Park nyumbani kwa Everton a.k.a The Toffie! wababe Manchester United walitoka vichwa chini baada ya kuanza msimu huu wa EPL kwa kipigo cha goli 1-0. Goli la washindi lilifungwa na kiungo mshambuliaji wa kibelgiji Mourane Fellaini katika kipindi cha pili baada ya timu hizo kumaliza kipindi cha kwanza bila ya kufungana. Fellaini alikuwa nyota wa mchezo huo kucheza kandanda safi na kuipa sehemu ya kiungo ya Manchester United waliokuwa wakitumia mfumo wa 4-5-1.
Manchester United iliyoanza kutumia wachezaji wake wapya wal;iosajiliwa msimu huu kama Shinji Kagawa aliyecheza mchezo mpaka mwisho alionyesha kuwa ni mchezaji wa kiwango kizuri na ataisaidia Man Utd msimu huu, pia kwa upande wa mchezaji aliyetengeneza vichwa vya habari duniani kote, Robin Van Persie alipata nafasi kuanza kuitimikia timu yake mpya katika dakika ya 68 ya mchezo huo. Katika mchezo huo Van Persie hakupata nafasi nzuri ya kuonyesha ubora wake. Akizungumza na bbc.com kocha wa United, Sir Alex Ferguson alisema " hatukumtumia vizuri Persie, yeye in mchezaji anayetaka kupenyezewa mipira kati kati ya mabeki wa kati wa timu pinzani lakini sis hatukufanya hivyo".
Nilicho kiona mimi ni kwamba Man Utd wana timu nzuri sana kama kikosi kilichopo kitaelewana kwa muda uliopo na pia Man Utd jana walikuwa wanacheza pasi fupi fupi lakini walikosa mtu wa kupigiwa penetration passes kwani Danny Welbeck aliyepewa jukumu hilo kama centrla striker alikua hakua akistick kwenye nafasi hiyo. Bado tuwape muda Man Utd wana kikosi bora msimu huu1
No comments:
Post a Comment